 |
Wanaowania tuzo ya kocha bora wa wanawake wa mwaka FIFA 2014 |
Kutoka kulia ni Ralf Kellermann alizaliwa 1968 huko magharibi ya Ujerumani aliyekuwa akicheza kama golikipa. Ralf Kellermann ni kocha anayeifua timu ya wanawake ya Ujerumani iitwayo Vfl Wolfsburg tangu 2008. Akiwa na Wolfsburg ameweza kushinda Bundesliga, DFB-cup, Uefa Women's Champions League kwa mwaka 2013 pekee.
Mwingine wakatikati ni mwanamama Maren Meinert aliyezaliwa 1973 alikuwa ni kiungo wa timu ya taifa ya Ujerumani ya wanawake. Kwasasa huyu mwanamama anafundisha timu ya taifa ya wanawake ya Ujerumani chini ya miaka 19. Kwa rekodi za UEFA ameweza kushinda mechi 50, droo mechi 4, shindwa mechi 5 katika mechi 59. Ambapo mwaka huu 2014 amweza kuzishinda timu za Czech Republic goli 4 kwa 1, Ukraine kapigwa goli 7 kwa nunge.
Wa mwisho ni Norio Sasaki mjapani aliyezaliwa 1958 huko Japan. Ni kocha mkuu wa timu ya wanawake ya Japani ambapo mwaka huu ameshinda kombe la wanawake bara la Asia(Women's Asian Cup).
 |
Wanaowania tuzo ya mwaka ya FIFA ya kocha bora wa wanawake |
Wakwanza kutoka kulia Carlo Ancelotti kiufupi amezaliwa mwaka 1959 huko Italia kwasasa ni kocha wa Real Madrid. Akiwa Madrid kwa mwaka 2013/2014 ameshinda Copa del Rey,Champions League, European Super Cup na akawa ni pekee kushinda Champions League/European Cup mara mbili kama mchezaji na mara 3 kama kocha.
Mwingine ni Joachim Low Mjerumani aliyezaliwa mwaka 1960. Kiufupi akiwa na timu ya taifa ya Ujerumani ameshinda Kombe la Dunia mwaka 2014 huko Brazil na pia akiweka rekodi ya kuifunga Brazil goli 7 kwa 1 huko Brazil
Mwite Diego Simeone amezaliwa mwaka 1970 huko Argentina. Kiufupi ni kocha wa Atletico de Madrid ambaye amefanikiwa kushika nafasi ya 3 La Liga 2012-2013 ikiwa ni rekodi toka waliposhinda ubingwa mwaka 1996, mwaka 2014 akiwafunga Real Madrid pale santiago kwa bao 1 bila ushindi ulioweka rekodi ya kushinda santiago toka 1999 na kocha Claude Ranieri. Akashinda ubingwa wa 10 wa La Liga 2013-2014 toka mwaka 1996. Akafika fainali za Bingwa Ulaya ambapo wakapigwa na Real Madrid.
 |
Wanaowania goli bora la mwaka la FIFA |
Wakwanza kutoka kulia ni mwanadada Stephanie Roche amezaliwa mwaka 1989 huko Jamhuri ya Ireland. Ni mshambuliaji wa timu ya wanawake ya taifa ya Ireland na mchezaji wa klabu ya Ufaransa ya daraja la kwanza ya ASPTT Albi. Roche alishinda goli hatari akiwa na klabu ya Peamount United dhidi ya Wexford Youth na kuangaliwa na watu wengi kwenye mtandao wa Youtube ambapo idadi imefikia idadi zaidi ya watu milioni 3
James Rodriguez mkolombia aliyezaliwa mwaka 1991 ni mchezaji wa timu ya taifa ya Kolombia na klabu maarufu ya Real Madrid. Alifunga goli maridadi dhidi ya Uruguay kombe la dunia kwa mguu wake wa kulia goli la kwanza kwneye mzunguko wa 2 wa Kombe la dunia mwaka 2014.
Robin Van Persie ni mdachi aliyezaliwa mwaka 1983 Netherland. Ni mchezaji na nahodha wa timu ya taifa ya Netherland na mchezaji wa Manchester United. Goli lake la ajabu alilifunga dhidi ya Spain kwa kupiga kichwa safi cha kujirusha.
 |
Wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa kike wa mwaka FIFA 2014 |
Nadine Kessler mwanadada hatari sana aliyezaliwa mwaka 1988 huko Ujerumani. Nadine anakipiga Vfl Wolfsburg na timu ya taifa ya wanawake ya Ujerumani. Kiufupi kwa msimu wa mwaka 2013-2014 ameshinda mwanasoka bora wa kike balani Ulaya na amisaidia Ujerumani kushinda UEFA Womens Championship na UEFA Women's Champions League akiwa na Vfl Wolfsburg.
'Marta' Marta Vieira Da Silva amezaliwa mwaka 1986 huko Alagoas Brazili.
Ni mchezaji anayekipiga huko Sweden katika clabu ya FC Rosengard na timu ya taifa ya Brazili. Kwa mwaka 2014 akiwa na klabu yake ya Rosengard amepachika goli 4 katika mechi 7. Kwa mwaka huu ameshinda ligi ya sweden iitwato Damallsvenskan.Ni mchezaji pekee pamoja na Birgit Prinz kufunga goli nyingi zaidi kwenye Kombe la Dunia kwa wanawake. Huko Brazili Marta anaitwa Pele mwenye sketi "Pele with Skirts"ambapo Pele mwenyewe alikubali kwakuwa ni mchezaji hatari sana.
Anaitwa Abby Wambach alizaliwa mwaka 1980 huko Marekani. Ni mchezaji wa klabu ya Western New York Flash. Kiufupi ni mwanadada aliyeshinda tuzo 6 za mcheza mpira bora nchini Marekani na alishinda pia mwaka 2013. Wambach ameweza kupachika goli 177 katika mechi 228 za kimataifa.
 |
FIFA Ballon D'OR |
Hakuna asiyemjua Cristiano Ronaldo.
Kipa bora kabisa sasa Manuel Neuer wa Timu ya taifa ya Ujerumani na klabu ya Bayern Munich. Anamiaka.Amesaidia kwa kiwango kikubwa timu yake ya Bayern Munich kuchukua ubingwa wa Bundesliga na timu ya taifa ya Ujerumani kutwaa kombe la dunia.
Hakuna asiyemjua Leonel Messi.
Washindi wa Ballon d'Or toka 2010 mpaka sasa.
|
2013: Cristiano Ronaldo (Real Madrid)
|
2012: Lionel Messi (Barcelona)
|
2011: Lionel Messi (Barcelona)
|
2010: Lionel Messi (Barcelona)
|