![]() |
Lionel Messi |
![]() |
Lionel Messi |
![]() |
Telmo Zarra |
Amekaririwa akisema "saivi nataka niweke nguvu kwenye kucheza mpira kufanya kazi yangu.....sipo hapa kushindana na Cristiano." akaendelea kwa kusema "zawadi na tuzo nazozipata ni vitu visivyo vya muhimu sana kuliko mpira wa miguu na hata hivo itakuwa ni vizuri kuwa kinara wa kupachika mabao katika ligi hii nzuri sana".
Messi pia akasema kuwa anafurahi kuwa chini ya kocha Luis Enrique. Barcelona sasa ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi kuu ya uhispania na wakiwa wameshinda michezo mitano na kudroo mchezo mmoja na timu ya Barcelona imeweza kucheza michezo sita ya laliga bila ya kuruhusu kutikiswa kwa wavu wao ambapo pia wamefunga goli 17. Barcelona inamchezo jumamosi hii na Rayo Vallecano ambao wanashikilia nafasi ya tisa na kitapigwa pale Estadio del Rayo Vallecano (de Vallecas Teresa Rivero) (Madrid)
Rekodi za Lionel Messi sasa
- Mpachika mabao namba 1 wa barcelona akiwa na goli 360
- Kuwa na tuzo nyingi za Ballon d'Ors 4
- Mchezaji mwenye hat tricks nyingi zaidi katika msimu mmoja 8
- Mchezaji mwenye goli nyingi zaidi za klabu bingwa Dunia 4...ambapo yupo sawa na Denilson
- Mchezaji mwenye goli nyingi zaidi za El Classico{Barcelona vs Real Madrid} 21
- Mchezaji aliefunga goli nyingi zaidi kwenye mechi moja kwenye mashindano ya UEFA Champions akiifunga Bayer Leverkusen goli 5
- Mchezaji aliyefululiza kufunga mabao katika kila mechi za Laliga ambapo amefululiza kufunga katika mechi 10 mfululizo
- Mchezaji aliyefunga goli nyingi zaidi katika msimu mmoja wa La Liga goli 50
- Mchezaji aliyepachika wavuni goli nyingi zaidi katika kalenda ya mwaka mzima goli 91
- Mchezaji alipewa tuzo nyingi za mfungaji bora katika mashindano ya UEFA Champions mara 4 akilingana na Gerd Muller.
No comments:
Post a Comment