Tuesday, 30 September 2014

Kocha wa Newcastle United Alan Pardew Mashakani

Kocha wa Newcastle United amebaki na swali kubwa na zito pale anapofikiria maisha yake ya ukocha akiwa na klabu hiyo. Kocha huyu alie na miaka 53 timu yake inashikilia nafasi ya pili kutoka mwisho wa msimamo wa ligi kuu ya Uingereza ambapo timu yake haijapata ushindi hata mmoja katika mechi sita ilizokwisha cheza ikiambulia droo tu Crystal Palace,Hullcity na Aston Villa na kuambulia pointi 3. Newcastle United ilifungwa bao moja na Stock City hiyo Jumatatu ya tarehe 29 mwezi wa 9 mwaka huu. Pardew amenukuliwa na vyombo mbalimbali akisema kua bado anapenda aendelee kuifundisha Newcastle United japokuwa kuna baadhi ya mashabiki washaanza kumkataa kocha huyo
Alan Pardew