 |
Sturridge akisaini mkataba Liverpool |
Daniel Sturridge ametia saini kwenye mkataba wake hii leo unao mbakiza zaidi Liverpool. Lakini picha iliyotolewa na Club ya Liverpool imeleta utata miongoni mwa mashabiki na waandishi wa habari za michezo. Katika picha hii Sturridge anaonekana akitia saini kwenye karatasi nyeupe isiyo na kitu. Labda mkataba wenyewe utatiwa saini baadae??....Ukiangalia nyuma mikataba kwa mfano ya Steven Gerrard kama inavonekana kwenye picha alisaini mkataba ambapo ukiziangalia hizo karatasi za mkataba zinaonesha maandishi tofauti na Sturridge. Mchezaji mwingine ni Kolo Toure ambaye nae alisaini mkataba makaratasi yakionesha maandishi. Inshu ya Daniel Sturridge inafananishwa na mlinzi Luis Alberto ambaye nayeye alionekana kwenye picha iliyotolewa na klabu akisaini katika karatasi nyeupe isiyo na maandishi ikiwa nyeupe pee kama inavoonekana kwenye picha ambapo mlinzi huyu aliambulia kwenda kwa mkopo Malaga...Mashabiki wa Sturridge waingiwa na hofu
Unafikiria nini kuhusu hili swala la Daniel Sturridge???
 |
Steven Gerard akiweka saini kwenye mkataba wake |
 |
Kolo Toure akitia saini kwenye mkataba wake |
 |
Luis Alberto akiweka saini kwenye mkataba wake |
No comments:
Post a Comment