Usain Bolt ameonekana jijini New York city, huku mashabiki wake wakiwa barabarani ili kutaka kumwona. Mjamaika huyu akitokea India alikua amevalia miwani mieusi na shati jeusi lililokua limeandika "Forever Faster". Waandishi wakamuuliza maswali kadhaa kama;
Unaweza vunja record yako ya mita 100?
"nafikiri naweza swala la msingi ni nisiwe na majeruhi nikipata mda mwingi ambao ntakua sina majeruhi basi naeza vunja record yangu."
Ni nani mshindani wako hasimu na unafiri nani anawezavunja record zako?
"sijui...sijui kama kuna mtu anaweza vunja record yangu ya dunia...kwakweli siwezi kusema ni nani. Mtu ambaye ni mshindani wangu nafikiri ni mwenzangu Yohan Blake kwasabu huwa namwona akifanya mazoezi na naona nia yake...pia na yeye akikaa mda mrefu bila ya kuwa majeruhi atakua mkimbiaji mkubwa sana."
We ni shabiki mkubwa wa Manchester United..Unafikiri Falcao ataisaidia klabu hiyo?
"Ni mchezaji mzuri...na nilikutana nae Ujerumani mwezi uliopita. Nilikua nikiongea nae na nikamtia moyo kuwa afanye kile anachokifanya kwasabu ni mchezaji mkubwa sana. kwakweli anaenda kuibadilisha ligi ya Uingereza."
Unafikiri Luis Van Gaal afanye nini ili Manchester United irudi kwenye mstari wake?
"Van gaal anajaribu kuingiza mfumo wake ni swala la wachezaji kufanya kile meneja anataka"
No comments:
Post a Comment