10 Nicolas Sebastien Anelka
Ni mfaransa aliyezaliwa mwaka 1979 huko Le Chesnay Ufaransa ambaye pia anamiaka 35 sasa. Anelka ameweza kucheza kwenye klabu za;
Paris Saint-Germain (1996-1997), Arsenal (1997-1999), Real Madrid ( 1999-2000), akarudi tena Paris Saint-Germain (2000-2002), akaenda kwa mkopo Liverpool (2001-2002), Manchester City (2002-2005), Fenerbahçe (2005-2006), Bolton Wanderers (2006-2008), Chelsea (2008-2012), Shanghai Shenhua (2012-2013) ambako alikua kocha mchezaji, baada ya mda mfupi akaenda kwa mkopo Juventus (2013), West Bromwich Albion(2013-2014) na sasa yupo Mumbai City 2014-.
09 Alexander "Andy" Cole

Andy Cole alizaliwa mwaka 1971 huko Nottingham Uingereza. Alitambulika sana kwa jina la Andy Cole miaka ya 1990 na 2000 akashauriwa atumie Andrew Cole. Cole ni mchezaji pekee wa pili kufunga magoli mengi zaidi katika ligi ya Uingereza BPL akitundika magoli 187 wakwanza akiwa ni Alan Shearer mwenye magoli 260. Cole amechezea klabu za;
Arsenal (1989-1992), kwa mkopo Fulham (1991), Bristol City (1992-1993), Newcastle United (1993-1995), Manchester United (1995-2001), Blackburn Rovers (2001-2004), Fulham (2004-2005),Manchester City (2005-2006), Portsmouth (2006-2007) na baada ya mda kidogo kwa mkopo Birmingham City (2007), Sunderland (2007-2008) na baada ya mda kidogo kwa mkopo Burnley (2008) na hatimaye 2008 akatimukia Nottingham Forest mpaka kustaafu.
08 Christian Vieri

Huyu ni muItaliano aliyezaliwa mwaka 1973 huko Bologna, Italia. Kwasasa anamiaka 41. Vieri amefanukiwa kucheza kwenye klabu 11 tofauti za ligi ya Italia yaani Serie A.1999 alikuwa ni mchezaji ghali zaidi duniani pale Inter Milan ilipomnunua kutoka Lazio kwa Paundi Milioni 32. Vieri ni moja ya wapachika mabao wa mda wote wa Italia(Italian strikers of all time). Vieri amekipiga;
Torino (1991-1992), Pisa (1992-1993), Ravenna(1993-1994), Venezia (1994-1995), Atalanta(1995-1996), Juventus(1996-1997), Atletico Madrid (1997-1998), Lazio(1998-1999),Internazionale(1999-2005), Milan (2005-2006), AS Monaco (2006) na mwaka huu huu Sampdoria, Atalanta(2006-2007), Fiorentina (2007-2008) na kustaafia Atalanta (2008-2009).
07 Adeola Oluwatoyin "Ade" Akinbiyi

Ade Akinbiyi alizaliwa mwaka 1974 huko Hackney, Uingereza na sasa ana miaka 40. Mmoja wa wazazi wake ni Mnigeria(NIGERIAN PARENT) na Mwaka 1999 alifanikiwa kuichezea Nigeria.Akinbiyi ni mchezaji wa kuhama hama ambapo alishawahi vunja rekodi ya club ya Leicester city kwa kununuliwa kwa paundi milioni 5. Ade ameweza chezea clabu za;
Norwich City (1993-1997), kwa mkopo Hereford United 1994 Ambapo mwaka huo wa 1994 tena kwa mkopo Brighton & Hove Albion, Gillingham (1997-1998), Bristol City (1998-1999), Wolverhampton Wanderers (1999-2000), Leicester City (2000-2002), Crystal Palace (2002-2003) tena kwa mkopo Stoke City mwaka 2003, Stoke City mwaka (2003-2005), Burnley (2005-2006), Sheffield United (2006-2007), Burnley (2007-2009), Houston Dynamo (2009), Notts County (2009-2010), na sasa kocha mchezaji huko Colwyn Bay toka mwaka 2013.
06 James Robert "Jimmy" Glass

Jimmy Glass ni Golikipa aliyezaliwa mwaka 1973 huko Epsom Uingereza. Anakumbukwa sana kwa kufunga goli la dakika za mwisho moja lililoiwezesha Carlisle United kubaki kwenye ligi mwaka 1999 ambapo ilipigwa kona yeye akatoka golini kwake mpaka kwa mpinzani na kutundika goli wavuni.Goli hilo lilisababisha uwanja kujaa mashabiki. Klabu alizochezea ni kama:
Crystal Palace (1989-1996) kwa mkopo Dulwich Hamlet mwaka 1989-1990, kwa mkopo Portsmouth (1995), kwa mkopo tena Gillingham (1995) na tena kwa mkopo Burnley (1996), Bournemouth
(1996-1998), Swindon Town (1998-2000), kwa mkopo Carlisle United (1999), Cambridge United (2000), Brentford (2000), Oxford United (2000-2001), Crawley Town (2001), kwa mkopo Brockenhurst(2001), Kingstonian (2001), Lewes (2001), Weymouth (2004). kwa sasa ni kocha wa magolikipa katika klabu ya Poole Town.
05 Rivaldo Vítor Borba Ferreira
Mbrazili maarufu sana kwa jina la Rivaldo alizaliwa mwaka 1972 huko Paulista, nchini Brazili. kwa sasa ni raisi wa klabu ya huko Brazili inayoitwa Mogi Mirim Esporte Clube. Rivaldo alikuwa ni kiungo mchezeshaji ambapo alikua anauwezo wa kucheza kama mshambuliaji wa pili. Moja ya vitu adimu vya kukumbukwa katika ulimwengu wa soka ni uwezo wa kupiga faulo kipekee zaidi kwa kuufanya mpira uende upande usiotarajiwa kwenda yaani "bending free kicks".Mwaka 1999 alishinda tuzo ya Ballon d'Or na mwaka 2014 alitangaza kustaafu soka. Hayo ni machache ya Rivaldo ambaye nae yupo kwenye orodha yetu ambapo ashacheza;
Santa Cruz(1991-1992), Mogi Mirim (1992-1994), kwa mkopo Corinthians (1993-1994),Palmeiras (1994-1996), Deportivo La Coruña (1996-1997), Barcelona (1997-2002), Milan (2002-2004), kwa mkopo Cruzeiro (2004), Olympiacos (2004-2007), AEK Athens (2007-2008), Bunyodkor(2008-2010), Mogi Mirim (2010-2011), kwa mkopo São Paulo (2011), Kabuscorp (2012), São (2013),na baadae kustaafu akiwa Mogi Mirim mkwa 2014.
04 Marcus Nathan Bent

NI Mwingereza mwingine aliyezaliwa 1978 huko Hammersmith London Uingereza. Marcus ameweza kucheza klabu tofauti tofauti nyingi sana na alishawahi kuwa mchezaji bora wa ligi kuu Uingereza mwaka 2002. Klabu alizokwisha cheza ni kama,
Brentford (1995-1998), Crystal Palace (1998-1999), Port Vale (1999),Sheffield United (1999-2000), Blackburn Rovers (2000-2001), Ipswich Town (2001-2004), kwa mkopo Leicester City(2003-2004), Everton (2004-2006), Charlton Athletic (2006-2008), kwa mkopo Wigan Athletic (2007-2008), Birmingham City (2008-2011), kwa mkopo Middlesbrough (2009-2010), kwa mkopo Queens Park Rangers (2010), kwa mkopo tena Wolverhampton Wanderers (2010-2011) kwa mkopo tena Sheffield United (2011) na mwisho kustaafu Mitra Kukar (2011-2012).
03 Trevor Junior Benjamin

Ni raia wa Jamaika aliyezaliwa Uingereza mwaka 1979. Baada ya kustaafu mpira Trevor akatengeneza bidhaa yake ya gloves inayoitwa Locust UK. Benjamini aliweza kuiwakilisha Jamaika mwaka 2002 pale ilipocheza na Nigeria jijini Lagos. Klabu alizokwisha chezea ni kama;
Cambridge United (1995–2000), Leicester City (2000–2005 ), kwa mkopo Crystal Palace (2001–2002 ), kwa mkopo Norwich City (2002), kwa mkopo tena West Bromwich Albion (2002), kwa mkopo tena Gillingham ( 2003), kwa mkopo Rushden
& Diamonds (2003–2004), kwa mkopo Brighton & Hove Albion (2004 ), kwa mkopo tena Northampton Town (2004–2005), Northampton Town (2005), Coventry City ( 2005 ), Peterborough
United ( 2005–2007), kwa mkopo Watford (2005), kwa mkopo tena Swindon Town (2006), kwa mkopo, Boston United
(2007) kwa mkopo Walsall (2007), Hereford
United (2007–2008), Gainsborough Trinity(2008), Northwich Victoria(2008), Hednesford Town(2008 ), Wellingborough Town(2008–2009), Kidsgrove Athletic(2009), Tamworth(2009), Harrogate Town(2009), Woking (2009), Sunshine George Cross (2010 ), Bedlington Terriers (2010) kwa mkopo Wroxham (2010) kwa mkopo Morpeth Town (2010), na hatimaye wakamnunua Morpeth Town (2010–2011).02 Stephen Edward "Steve" Claridge

Ni mwingereza aliyezaliwa mwaka 1996 huko Portsmouth na anaumri wa miaka 48. Steve kwa sasa ni mchambuzi wa mpira wa BBC Sports na kocha asiye rasmi. Steve alistaafu rasmi soka mwaka 2007 na alishawahi kuwa kocha wa Portsmouth mwaka 2000-2001, Weymouth mwaka 2003-2004 na Millwall mwaka 2005. Nae yupo kwenye hii orodha kwakucheza kwenye klabu za;
Fareham Town(1983–1984), Bournemouth(1984–1985), Weymouth(1985–1988), Crystal
Palace (1988), Aldershot(1988–1990), Cambridge
United(1990–1992), Luton Town(1992), Cambridge United(1992–1994), Birmingham
City(1994–1996), Leicester City(1996–1998) kwa mkopo Portsmouth (1998), Wolverhampton (1998) Wanderers,Portsmouth kwa mkopo Millwall, Millwall, Weymouth, Brighton
& Hove Albion, kwa mkopo Brentford ,Wycombe Wanderers Wycombe Wanderers, Millwall, Gillingham, Bradford City kwa mkopo Walsall, Bournemouth, Worthing, Harrow
Borough, Weymouth na baadae Gosport
Boroug
01 John Burridge
Ni golikipa mwingereza aliyezaliwa mwaka 1951 huko Workington. John ilimchukua miaka 30 kuweza kucheza katika klabu 29 tofauti tofauti ulimwenguni na alikua kocha mchezaji wa Blyth Spartans mwaka 1997 na hizi ni klabu alizoweza kuzichezea,
Workington(1969–1971)
kwa mkopo Blackpool (1971), Blackpool 1971–1975,
Aston Villa1975–1978 kwa mkopo Southend United (1978), Crystal Palace1978–1980,
Queens Park Rangers1980–1982, Wolverhampton Wanderers1982–1984 kwa mkopo , Derby
County (1984), Sheffield United1984–1987, Southampton1987–1989, Newcastle
United1989–1991, Hibernian1991–1993, Newcastle United1993, Scarborough1993, Lincoln
City1993–1994, Enfield 1994, Aberdeen1994, Newcastle United1994, Dunfermline Athletic1994,
Dumbarton1994, Falkirk1994, Manchester City1994–1995, Notts County1995, Witton
Albion1995, Darlington1995, Grimsby Town1995–1996, Gateshead1996, Northampton
Town1996, Queen of the South1996, Purfleet1996, Blyth Spartans1996, Scarborough1996
NA HATIMAYE Blyth Spartans1997.
Source:sportscas.blogspot.com
No comments:
Post a Comment