Tuesday, 4 November 2014

NGASA, MUBELE NGOMA DROO KWA MAGOLI KLABU BINGWA AFRIKA

Uncle Ngassa amemaliza kinara baada ya kufunga mabao sita na kufungana na Ndombe Mubele wa AS Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Haythem Jouini wa Esperance de Tunis ya Tunisia na El Hedi Belameiri wa ES Setif ya Algeria.
Ni baada ya Ligi ya Mabingwa Afrika kufikia tamati wikiendi iliyopita na ES Setif kutangazwa mabingwa wapya wakibebwa na bao la ugenini kutokana na matokeo ya sare bao 1-1 mchezo wa Algeria na sare mabao 2-2 mchezo uliochezwa Kinshasa.


MABINGWA WALIOPITA
2014: ES Setif (Algeria)
2013: Al-Ahly (Egypt)
2012: Al-Ahly (Egypt)
2011: ES Tunis (Tunisia)
2010: TP Mazembe (DRC)
2009: TP Mazembe (DRC)
2008: Al-Ahly (Egypt)
2007: Etoile du Sahel (Tunisia)
2006: Al-Ahly (Egypt)
2005: Ah-Ahly (Egypt)
2004: Enyimba (Nigeria)
2003: Enyimba (Nigeria)

No comments:

Post a Comment